SERIKALI KUONGEZA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA MAZAO YA MAFUTA.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Singida. Katika mwaka 2021/2022 Serikali imeongeza bajeti ya Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) kutoka Shilingi bilioni 7.35 mwaka 2020/2021 hadi Shilingi bilioni 11.63 mwaka 2021/2022.Vilevile, bajeti ya Wakala wa Mbegu wa Taifa (ASA) kutoka bilioni 5.42 mwaka 2020/2021 hadi Shilingi bilioni 10.58 mwaka 2021/2022 ili kuongeza upatikanaji wa mbegu bora